|
Kumetokea ajali ya aina yake jioni hii mjini Shinyanga ambapo gari
ndogo aina ya RAV4 yenye namba za usajili T167 ATW imegonga nyumba katika mtaa
wa Mnara wa Voda mjini Shinyanga.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 11 jioni ambapo mashuhuda
wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na
watu wawili wanaodaiwa kuwa walikuwa wanajifunza kuendesha tena kwa mwendo kasi
ndipo gari ikawashinda na kupoteza mwelekeo kisha kugonga nyumba hiyo na
kusababisha uharibifu mkubwa.
Gari hiyo imeharibu vibaya Chumba cha mpangaji aliyejulikana
kwa jina la Fatuma kuharibu vifaa mbalimbali zikiwemo TV katika chumba hicho na
chumba cha jirani cha Fundi Sonara aliyejulikana kwa jina la Ally Salum.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na
wahusika wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na mmliki wa gari
hiyo bado hajajulikana.
Mwandishi
wetu Kadama Malunde,alifika eneo la tukio,ametuletea picha zifuatazo
|
|
Gari ikiwa imegonga nyumba hiyo |
Gari ikiwa chumbani
|
Muonekano wa gari hiyo kwa ukaribu |
|
Askari
wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio wakiwajibika
|
Gari ikiwa ndani ya chumba |
|
Mashuhuda
wa tukio hilo wakiwaeleza askari polisi wa
usalama barabarani namna ajali hiyo ilivyotokea
|
Katikati
ya hiyo miti ndipo ilipopita gari hiyo ikiwa katika mwendo kasi kisha kugonga
nyumba hiyo |
|
ndani ya chumba cha mpangaji Fatuma
Chumba
cha mpangaji Fatuma kikiwa kimeharibika vibaya
|
Fundi
Sonara Ally Salum akionesha ilipokuwa TV yake iliyoharibika |
|
Fundi
Sonara Ally Salum akionesha akitafakari jambo nje ya chumba chake |
|
Askari wakitafakari namna ya kuiondoa gari hiyo eneo la tukio |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio baada ya gari hiyo kuondolewa kwenye chumba |
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni