TANGAZO

TANGAZO

Jumamosi, 6 Juni 2015

WAISLAMU NCHINI UGANDA WALALAMIKA NJAMA JUU YAO

Waislamu nchini Uganda walalamikia njama dhidi yao

Waislamu nchini Uganda walalamikia njama dhidi yao
Mufti Shaban Ramadhan Mubajje wa Uganda amelalamikia vikali mauaji yanayofanywa mara kwa mara dhidi ya masheikh nchini humo.
Gazeti la kila siku la New Vision la nchini Uganda limemnukuu Mufti Mubajje akisema kuwa, kuna watu wana nia ya kueneza fitna na mizozo kati ya Waislamu na kuongeza kwamba, mauaji hayo yalianza kama "mchezo," lakini sasa yamekuwa ni hatari kwa Waislamu. Amesisitiza kwamba, inasikitisha kuona kuwa Waislamu wa Uganda wameshapoteza masheikh zaidi ya watano.
"Ilianza kama mchezo lakini sasa imekuwa ni tishio kubwa. Tunapaswa kuwa macho na kuguswa na suala hilo kama Waislamu," amesema.

Sheikh wa karibuni kabisa kuuawa nchini Uganda alikuwa ni Sheikh Abdul Rashid Wafula aliyepigwa risasi tano kifuani na kuuawa katika mji wa Nakalole huko Mbale, mwezi uliopita.
Sheikh Mustafa Bahiiga aliuawa mwezi Disemba mwaka jana katika msikiti wa Bwebajja, katika barabara ya Entebbe, wakati Sheikh Abdul Qadir Muwaya naye aliuwa nyumbani kwake huko Mayuge kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Mwaka 2012 pia, viongozi wawili wakubwa wa Waislamu, Sheikh Abdul Karim Ssentamu na Hajj Abubakar Kiweewa waliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Mufti wa Uganda amemlaumu Mkuu wa Polisi wa nchi hiyo Jenerali Kale Kayihura akisema kuwa amekataa kuonana naye akikwepa kujadiliana naye suala hilo hilo la kuuawa viongozi wa Kiislamu.
Sheikh Mubajje ameitaka mahakama ya Uganda ifanye haraka kuwapandisha kizimbani watu waliotiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo na adhabu kali itolewe kwa watu watakaopatikana na hatia ili iwe funzo kwa watu wengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni