TANGAZO

TANGAZO

Jumamosi, 6 Juni 2015

SITTA,LOWASSA WAANZA KWA MBWEMBWE


Mwanza/Dodoma/Dar. Makada wanaoomba kupitishwa na CCM kuwania urais jana walianza kusaka wadhamini kwa staili ya aina yake baada ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kuibuka na basi la kifahari atakalotumia kuzunguka mikoani, huku Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akitua Mwanza kwa ndege.
Sitta, ambaye alitangaza nia yake ya kuwania urais juzi, jana alikuwa miongoni mwa makada watatu waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwenye ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma kabla ya kuanza kusaka wadhamini.
Wengine waliochukua fomu ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Titus Kamani na waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Wanaochukua fomu hizo za CCM wanatakiwa kutafuta wanachama kwenye mikoa 15, huku 10 ikiwa ya Tanzania Bara na mitano ya Zanzibar na wanatakiwa wapate wadhamini 450 kwa mikoa hiyo na mwisho wa kurudisha fomu ni Julai 2 wakati vikao vya mwisho kuteua mgombea vitafanyika Julai 12.
Sitta, ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alianza kutafuta wadhamini mjini Dodoma na alitarajiwa kuendelea na kazi hiyo kwenye mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe na Mbeya, lakini kilichovutia zaidi ni basi alilosema amekodi aina ya Yutong ambalo lina sehemu ya kukaa kama sebule.
Sitta na basi lake
Sitta alifika katika jengo la ofisi hizo za CCM akiwa ndani ya basi hilo aina ya Yutong, ambalo alisema sehemu yake ya ndani ilibuniwa na mwanaye.
Ndani ya basi hilo kuna kochi moja kubwa ambalo linaweza kutumika kama kitanda, kiti cha ofisini na meza ndogo iliyopambwa na picha yake na maneno “viwango mwaka 2015-2020”.
“Hivi vyote ni vitu vya nyumbani kwangu, kijana wangu anaitwa Ben alibuni namna (ya kuviweka kwenye basi). Sikutumia gharama yoyote zaidi ya kukodisha basi,” alisema Sitta akiwa ndani ya basi hiyo na mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Rage.
Alisema aliamua kutumia basi hilo la abiria ili apunguze gharama za utafutaji wa wadhamini katika mikoa 18 anayotaka kwenda kuwatafuta.
“Unajua nina marafiki zangu kama 11 nataka niwe nao sasa kutumia usafiri wa magari ni gharama ndio maana tukaamua kufanya hivi,” alisema Sitta na kuongeza kuwa katika safari zake hizo atakuwa akisafiri usiku.


Vipaumbele vya Sitta
  ENDELEA KUTEMBELEA THOMAS WIKESI BLOGSPOT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni