AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
Simba
Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza mawasiliano na
wadau wake mbalimbali hususani; wanachama, wapenzi, vyombo vya
habari na wadau wengine muhimu.
Akizungumza
wakati wauzinduzi huo Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika
dunia na zama za utandawazi tovuti ndio na mitandao ya jamii
ndio njia kuu ya mawasiliano. Sisi tuliliona hili na leo hii
nafurahi kuwa Simba Sports Club itazindua rasmi tovuti yake
ambayo itakuwa jukwaa kuu la mawasiliano na utoaji wa taarifa zake
za club ya Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu
zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu tovuti yetu’’.
AfisaMtendajiMkuuwa
EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona
Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa
wadau wake taarifa mbalimbalibali pia itatumika kwa ajili ya uuzaji
wa vifaa vya Simba, Bidhaa mbalimbali mpya na muhimu zaidi
kuwaunganisha wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kutumia
mitandao ya jamii iliyo rasmi ya Simba Sports Club’’.
Mkutano
huo wa wandishi wa habari ulitumika kutaarifu Wanachama,
Wapenzina Vyombo vya habari juu ya kocha mpya wa Simba.
Alizungumza wakati wakumtambulisha kocha mpya wa Simba, Rais
Aveva alisema ‘’Baada ya kupitia vyeti na maombi ya makocha
mbalimbali, Napenda kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia kwenye
mkataba wa kuifundisha na kocha Dylan Kerr raia wa
Uingereza. Ni kocha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30,
akiwa amefanya kazi Nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza,
Scotland, Vietnam na AfrikayaKusini’’.
Aliendelea
kusema ‘’Tunaamini ujuzi na uzoefu wake wa ukocha na pia kama
mchezaji wa kiwango cha juu utakuwa chachu ya kuifanya Simba
ifanye vizuri’’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni