TANGAZO

TANGAZO

Alhamisi, 18 Februari 2016

VIDEO: Serikali imeamua haya kuhusu viwango vipya vya ufaulu kwa wanafunzi…


February 18 Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2015, jambo lingine kubwa lililopewa nafasi ni hili la viwango vya ufaulu vilivyotangazwa kuanza tena kutumika.
Hapa chini kwenye hii video nakusogeza karibu na Katibu mtendaji wa baraza la mitihani Tanzania NECTA Dk. Charles Msonde.

Sentensi sita za NECTA kuhusu matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2015 .


February 18 baraza la mitihani Tanzania NECTA wametangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2015 yafuatayo ni maneno matatu waliyosemwa na katibu mtendaji wa baraza la mitihani Tanzania NECTA Dk Charles Msonde.
“Katika mkutano maalum wa baraza wa 110 uliofanyika February 17 2016, baraza la mitihani Tanzania lilipitia taarifa ya matokeo ya kidato cha nne na maarifa uliofanyika tarehe 2 hadi 27 November 2015 na kuidhinisha kutangaza rasmi kwa matokeo hayo katika mitihani ya kidato cha nne 2015”

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015 YAKO HAPA

Kama ujapata matokeo kidato cha nne mtu wangu wa nguvu nimekusogezea hapa

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

CSEE 2015 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES

Alhamisi, 11 Februari 2016

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 12 2016 kwenye Udaku, Hardnews na michezo


February 12 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu..

Jumatano, 10 Februari 2016

Kiasi Cha Fedha Atakachokuwa Akilipwa Mourinho Man Utd Na Muda Wa Mkataba Wake Watajwa

Tetesi za kupewa kwa Jose Mourinho na klabu ya Manchester United zinazidi kushika hatamu kila dakika.
 
Gazeti la kila siku El Confidencial leo limeripoti taarifa za ndani za mkataba unaosubiriwa kusainiwa baina ya Jose Mourinho na waajiri wake wapya Manchester United.
Taarifa za ‘Special One’ kubeba mikoba ya Van Gaal zimechapishwa na kila chombo cha habari huko England asubuhi ya leo.
Vichwa vya habari vya magazeti vimeandika kwamba: Jose Mourinho amewaambia marafiki wa karibu kwamba atakuwa boss mpya wa United kuanzia msimu ujao.

FC BARCELONA WATINGA FAINALI KWA KISHINDO BAADA YA KUWEKA REKODI HII...................

Sare ya bao 1-1 iliyoipata FC Barcelona dhidi ya Valencia jana usiku katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Copa del Rey siyo kwamba imeiwezesha kutinga fainali ya michuano hiyo pekee bali pia imeiwezesha miamba hiyo ya Catalunya kuweka rekodi ya kucheza michezo 29 bila kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano yote na kuvunja rekodi yake ya mwaka 2010/11 ya kucheza michezo 28 bila kupoteza.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 11 2016 kwenye Udaku, Hardnews na michezo


February 11 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu..

TUTARAJIE MABADILIKO HAYA KATIKA KOMBE LA MABINGWA BARANI ULAYA UEFA..............


Vilabu vikubwa barani ulaya vinajadili mbinu za kufanyia marekebisho ligi kuu ya mabingwa barani humo.
Vilabu hivyo hata hivyo vimepuzilia mbali uvumi kuwa wanapendekeza kuvunjwa kwa ligi hiyo na kuanzishwa kwa ligi mbadala ya 'Super League'.

Muungano wa vilabu barani humo European Clubs' Association (ECA) linasema kuwalinapanga kufanya marekebisho hayo kwa ushirikiano na UEFA ifikapo mwaka wa 2018.

Azam FC kuzialika Tanzania TP Mazembe, Zesco United


COVER

Habari na mtandao wa AzamFC:
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuwa mwenyeji wa michuano maalumu ya kimataifa ya timu nne itakayofanyika mwanzoni mwa mwakani.
Michuano hiyo ni ile waliyoenda kushiriki jijini Ndola Zambia hivi karibuni na kutwaa ubingwa, ambapo imeanzishwa kwa muungano wa klabu tatu, Azam FC, TP Mazembe na Zesco United.

Milioni 700 zimepotea Air Tanzania, Maamuzi ya Waziri wa Uchukuzi ni haya…(+Audio)

Serikali imebaini wizi wa takribani Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel ya Komoro. 
Hapa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa anatoa maelezo yote, unaweza kumsikiliza

Jumapili, 7 Februari 2016

MATOKEO YA GEMU ZOTE ZA VPL LEO, YANGA, SIMBA, AZAM ZASHINDA, ANGALIA SASA MSIMAMO ULIVYO

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/09/vpla-426x360.jpgMshambuliaji wa yanga Saimon Msuva hii leo ameiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa goli 4-0 mbele ya JKT Ruvu yeye akifunga goli 2 katika ushindi huo mnono, unaowaweka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom kwa pointi 1 zaidi ya Simba SC na Azam FC.

Katika mchezo huo yanga sc walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0, zilizofungwa na Saimon Msuva katika dakika ya 12 na Issoufou Bobackari katika dakika ya 43 ya mchezo

ANGALIA PICHA KIBAO ZA USHAHIDI JINSI ZOUMA ALIVYOUMIA JANA KWENYE GEMU DHIDI YA MAN UNITED.. GET WELL SOON......


Beki wa kati wa Chelsea, Kurt Zouma ameumia goti lake upande wa nyuma baada ya kutua vibaya wakati akirejea chini alipokuwa akiwania mpira wa juu katika mechi dhidi ya Man United iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.

Ijumaa, 5 Februari 2016

HII NIORODHA YA MAWAZIRI VIVULI


 ORODHA YA MAWAZIRI VIVULI;

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI - Mhe. Jaffar Michael. 

2. Waziri wa Nchi Utumishi - Mhe. Ruth Molel. 

3. Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira - Mhe. Ally Saleh (Alberto).

4. Waziri wa Nchi, Sera na Bunge - Mhe. Ester Bulaya.

5. Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe. Halima James Mdee.

6. Waziri wa Ujenzi - Mhe. James Francis Mbatia.

7. Waziri wa Nishati na Madini - Mhe. John John Mnyika.

8. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda - Mhe. Peter Msigwa.

Taarifa kamili iliyonifikia kutokea bungeni kuhusu Watanzania kuvamiwa na kuuawa India…(+Audio)



Stori ya Wanafunzi wa Tanzania kuvamiwa na kupigwa huku mmoja wa wasichana akivuliwa nguo na kutembezwa barabarani imechukua headline nyingi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari haswa hapa nchini, uzito wa tukio hili umefika bungeni Dodoma, Na hapa Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga ana haya ya kusema.
Jana nilitoa taarifa ya awali kuhusu wanafunzi wa Kitanzania walipingwa na msichana mmoja alivuliwa  nguo na kutembezwa barabarani nchini India, taarifa tulizozipata ni kweli kitendo kilitokea

UNAJUA KINACHOMUWEKA BENCHI MAGURI? MWENYEKITI WA STAND ATUMBUA JIPU

Elius Maguri, Mshambuliaji wa Stand United anatesa baada ya kutemwa MsimbaziElius Maguri, amejikuta akichezea mkeka ndani ya kikosi cha Stand United licha ya kuwa kwenye kiwango bora kwa sasa
Mshambuliaji wa Stand United Elius Maguli siku za hivi karibuni amekuwa haonekani dimbani kutokana na kuchezea mkeka ndani ya kikosi cha Stand United chini ya kocha mfaransa Patrick Liewig.

STORY MPYA KUHUSU CHANONGO NA UBWA NDANI YA TP MAZEMBE

ddKimya kimetanda tangu wachezaji wa Stand United Haruna Chanongo na Hassan Ubwa walipokwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR na hatimaye kurejea nchini kimyakimya bila klabu ya Stand kuwajulisha watanzania majibu ya wachezaji hao kama wamefuzu au wamekwama.

Hii hapa namba ya waliokamatwa kwa kuchoma mali za watuhumiwa wa mauji ya Diwani Muleba Kagera…(+Audio)


Ripoti kutokea Mkoa wa Kagera kuhusu lile tukio la mauaji ya Diwani aliyevamiwa na watu usiku akitazama Habari nyumbani kwake, Wananchi waliamua kuchoma mali za watuhumiwa wa mauaji, Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi, Augustine Ollomi kwenye sentensi zake; – RPC Augustine Ollomi
Ni kweli kuna watu 13 tunawashikiria wanawake watatu na wanaume 10 kwa tuhuma za kuharibu mali za watuhumiwa wa mauaji kwa madai walihusika na mauaji ya Diwani wa Kata ya Kimwani Wilaya ya Muleba Kagera, Syliveste Mulinga ( CUF ), ;- RPC Ollomi

BABA WA NEYMAR AFICHUA DAU LILILOTENGWA NA MAN UTD KWA AJILI YA MWANAE

Neymar-in-court
Baba mzazi wa mchezaji wa Barcelona, Neymar Jr wiki hii amefichua siri juu pesa ya ambayo klabu ya Manchester United waliyoitenga msimu uliopita kutaka kumsajili mtoto wake kutoka Barcelona,  huku wakiwa tayari kukidhi buyout clause iliyowekwa na Barcelona ya pauni 145m ili kumnasa mbrazili huyo.
Neymar Snr ambaye amemsindikiza mwanae katika kesi inayowakabili ya kutoweka wazi kiasi sahihi cha pesa ambayo FC Barcelona walitoa kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Santos ya Brazil, amesema kuwa Manchester United walitenga mezani mamilioni hayo ya fedha kumtaka mwanae lakini akasisitiza kuwa hajui kitakachotokea mbeleni,  ila bado kijana wake ana mkataba wa misimu 2 na ana furaha  Nou Camp.

Alhamisi, 4 Februari 2016

INASIKITISHA… Jamaa kaota mizizi kwenye mwili wake


Moja ya ripoti iliyonifikia kutokea nchini Bangladesh ni hii ya jamaa kuugua ugonjwa wa kuota mizizi katika sehemu za viungo vyake vya mwili.
Abul Bajandar  alianza kupata hali miaka 10  iliyopita, ugonjwa huu unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi au “ugonjwa wa binadamu mti”.
Serikali ya Bangladesh kupitia kwa Waziri wa afya Mohammad Nasim imesema itagharimia upasuaji wa kijana huyo.

MESSI AWEKA REKODI NYINGINE KWENYE MAISHA YAKE YA SOKA

Messi-500

 Messi ameandika rekodi nyingine tena kwenye maisha yake ya soka wakati FC Barcelona ikiiangushia kipondo ‘heavy’ timu ya Valencia kwenye mchezo wa kombe la mfamle Hispania maarufu kama Copa del Rey.

VPL: SIMBA MWENDO MDUNDO, YANGA YACHECHEMEA, MATOKEO, MSIMAMO NA WAFUNGAJI YAPO HAPA

SIMBA SC imejiweka sawa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga Mgambo JKT mabao 5-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
http://1.bp.blogspot.com/-mYophk0enlc/VjG3Q2q8iOI/AAAAAAAAq2I/2JFGgKDo1Kw/s640/VPL-logo.jpg
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 39 baada ya kucheza mechi 17, sasa ikiwa inazidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Yanga SC walio kileleni, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 39 pia.

Jumatano, 3 Februari 2016

Baba yake Neymar kataja kuwa imemfikia ofa ya pound milioni 144.4 kwa ajili ya Neymar, The Sun wataja klabu inayomtaka


Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar, bado yupo kwenye headlines kuhusiana na suala lake la usajili kutoka Santos kujiunga FC Barcelona mwaka 2013, kudaiwa kuwa na magumashi kiasi cha yeye kufikishwa mahakamani kutoa ushahidi.