TANGAZO

TANGAZO

Jumapili, 23 Agosti 2015

FIFA YAKAA KITAKO NA WADHAMINI WAO KUJADILI MASWALA ;YA RUSHWA

Rais wa Fifa, Sepp Blatter


Shirikisho la kandanda duniani Fifa, limekutana na baadhi ya wadhamini wake wakubwa kujadili uchunguzi wa maswala ya rushwa.

Mamlaka za Marekani na Uswisi zinachunguza madai ya utoaji na upokeaji rushwa kwa viongozi wa juu wa shirikisho hilo.
Wadhamini waliokutana na shirikisho hilo ni AB InBev, Adidas, Coca-Cola, McDonald pamoja na Visa.

Ambapo shirikisho hilo la kandanda likakubaliana na wadhamini hao kufanya kazi kwa uwazi, mageuzi, na kushirikiana na washirika wake kwa ukaribu.
Katika taarifa ya pamoja ya wadhamini hao ilisema: ni matarajio yao watafanya mageuzi imara, na wataendelea kushirikana na Fifa.".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni