Kocha huyo wa Arsenal amemsajili Peter Cech pekee kama mchezajia aliyeongeza nguvu kikosini licha ya kuwa mitandao mingi ya Ulaya inajua klabu ya Arsenal itafanya usajili mkubwa msimu huu licha ya Wenger kutokubali kuwa ana mpango wa kusajili.
Hata baada ya kufungwa mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Uingereza na klabu ya West Ham United ya Uingereza bado Wenger anakikri kuwa walikuwa dhaifu dhidi ya West Hamlakini haamini kama ufumbuzi wa ubovu wa kikosi chake utapatikana kwa kusajili.
“Hatukuwa na kiwango kizuri na cha kuvutia, kimsingi West Ham walicheza vizuri na hongera kwao natumaini tutarejea katika kiwango chetu haraka. Naweza rudia tena kama nilivyosema awali kama ufumbuzi pekee wa tatizo utakuwa ni kusajili tutafanya hivyo lakini baada ya kufungwa kama hivi sio muhimu kuangalia ufumbuzi wa tatizo nje ya kikosi”>>>Wenger
karibu tena katika blogs hii
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni