Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya
Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni
mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi
kuinadi ilani ya CCM.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa
mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la
Iramba Magharibi. Mbunge Nkenge CCM aliyemaliza muda wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCM Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa
tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la
Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa
tena, Lazaro Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya
wananchi baada ya kutua na helkopta. Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto)
wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi.
Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku. wa
Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge
Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni
mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi
kuinadi ilani ya CCM. Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba.
Na Joachim Mushi, Singida
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba
kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza
wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu katika mikutano yake
inayoendelea ya kuinadi ilani ya CCM.
Nyarandu ambaye jana alishuka kwa helkopta ya kukodi Jimboni kwake ikiwa
ni muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za
wanaCCM na wananchi katika mkutano huo.
Kama hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge alitumia helkopta hiyo kwenye
mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya Jimbo la Iramba Magharibi.
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba
Magharibi mkoani Singida, Bi. Suluhu aliwaomba wananchi kuipigia kura
CCM kwani ndani ya ilani yake imepanga kufanya mambo mazuri kwa
maendeleo ya mkoa huo.
Alisema endapo watachanguliwa watajenga kiwanda kikubwa cha kusafishia
mafuta ya alizeti jambo ambalo litaongeza thamani ya mazao kwa wakulima
wa eneo hilo.
Aliongeza kuwa mbali na kiwanda hicho kikubwa kuwanufaisha wakulima pia
kitatoa nafasi za ajira kwa vijana ambapo jumla ya wafanyakazi 600
watapata ajira ndani ya kiwanda hicho, alisema baada ya Serikali ya
awamu ya nne kujenga shule za Sekondari za kata za kutosha na maabara
ilani mpya ya CCM imepanga kushughulikia suala la vifaa vya maabara hizo
ili ziweze kutumika kwa ufasaha.
Bi. Suluhu alisema Mkoani Singida imepanga kujenga hospitali kubwa ya
rufaa ambayo itakuwa ikitoa huduma katika mkoa huo na mikoa ya jirani,
pamoja na ujenzi wa barabara ya Ndago.
Aidha akihutubia katika Mkutano mwingine Wilaya ya Ikungi aliahidi
kufanya jitihada za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili
kusongeza huduma kubwa za afya kwa wanaIkungi, pamoja na kuvipatia umeme
vijiji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo kupitia mradi wa Wakala
wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya pili.
Aliongeza kuwa licha ya maeneo ya mikoa ya singida kukabiliwa na tishio
la ukame aliwahakikishia hakuna raia atakayekufa njaa katika maeneo
hayo. "...Serikali imejipanga na ghala la kuhifadhi chakula lina akiba
ya kutosha, hivyo niwahakikishie hakuna mwanakijiji ambae atakufa kwa
njaa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba
ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza
jimboni hapo alisema ilani ya CCM imepanga kutekeleza miradi ya maji
katika Vijiji vya Mgundu, Kinampanda, Makunda pamoja na vijiji vingine
vinavyokabiliwa na kero ya maji.
Alisema baadha ya mradi wa ujenzi wa shule za Sekondari za kata
kufanikiwa serikali itakayoundwa na CCM imepanga kusimamia ujenzi wa
mabweni ili kuwanusuru watoto wanaotembea umbali urefu kwenda shuleni
pamoja huku wasichana wakikabiliwa na changamoto za kubebeshwa mimba na
kukatishwa masomo yao.
Mwingulu aliwataka wananchi kutochagua vyama vingine kwani havina hoja
za msingi na vingine vinaazima hadi wagombea ili viweze kuwasimamisha.
Bi. Suluhu anaendelea na ziara yake ambapo sasa anaelekea Mkoa wa Dodoma
akiinadi ilani ya CCM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni