TANGAZO

TANGAZO

Jumatatu, 3 Agosti 2015

Msuva? Hapana, kama Niyonzima sawa

STRAIKA wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’, amebainisha kuwa itakuwa ngumu kwa winga wa Yanga, Simon Msuva, kucheza Simba kutokana na staili yake isiyovutia, lakini ni rahisi zaidi kwa Haruna Niyonzima au Salum Telela kutua Msimbazi na kung’ara.
Mgosi alisema kati ya viungo wanaotamba nchini, Niyonzima na Telela ndiyo wachezaji pekee wa Yanga wanaoweza kuichezea Simba na kutamba kwa utamaduni wa soka la Simba, lakini siyo kwa mchezaji kama Msuva aliyedai haendani na aina ya soka la Msimbazi
.
“Simba ina falsafa ya kipekee. Licha kwamba timu huwa ikisaka matokeo, ila sera yao ni kucheza soka la pasi nyingi na la kuvutia kwa kuwa wanalenga kuwaburudisha mashabiki. Sasa kwa Msuva hawezi kwani soka lake la kukimbia pembeni halichezwi sana Simba,” alisema.
“Niyonzima aanajua kuburudisha lakini pia ana uwezo wa kuichezesha timu pamoja na kukaba. Kimsingi ni mchezaji mwenye vigezo vya kuwa Simba sambamba na kiungo Salum Telela,” alifafanua Mgosi.
Mgosi amerejea Simba miaka mitano tangu alipoiacha
CHANZO;MWANA SPORT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni