Mwenyekiti wa NCCR – Mageuzi, James
Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, ameonesha kutoridhika
na uamuzi unaofanywa na jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yake
akidai kuwa hufanya upendeleo viongozi wa ngazi za juu wa CCM huku
akimtolea mfano rais wa awamu ya pili, Benjamini Mkapa.
Akiongea na waandishi wa habari jana,
Mbatia alieleza kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi,
Suleiman Kova ameshindwa kumchukulia hatua za kisheria Mzee Mkapa kwa
kosa lile lile lililowahi kufanywa na askofu Josephat Gwajima
aliyechukuliwa hatua kali.
“Gwajima alitoa kauli zilizosemekana
kuwa ni za kuudhi dhidi ya Kadinali Pengo, lakini Kadinali alisema
amemsamehe. Pengo alimsamehe hadharani laini vyombo vya dola
vilimfungulia kesi mahakamani,” alisemaa Mbatia.
“Juzi tumesikia matusi mabaya kuliko ya
Gwajima yakitolewa na viongozi wa CCM akiwemo Mkapa, kwa nini yeye
hajakamatwa. Kwanini Kova hajamkamata Mkpaa na kumfungulia mashtaka
dhidi ya uchochezi,”alisema.
Mbatia alilitaka jeshi la Polisi
kuhakikisha linatenda haki kwa kila mmoja na kwamba sheria isipofuatwa
vizuri bila ubaguzi inaweza kulipasua taifa.
Aliwataka wanachama wa Ukawa kuwa
watulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi na kuwa na uvumilivu pia kwa
kuwa utulivu na amani ya Taifa ni kitu bora zaidi ya vyama vya siasa.
Katika hatua nyingine, Mbatia
alisisitiza kuwa ratiba ya Ukawa kufanya uzinduzi katika uwanja wa
Jangwani iko pale ingawa Serikali imelikataa ombi lao la kuutumia uwanja
huo kwa madai kuwa tayari umechukuliwa na mtu mwingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni