Mchezaji wa Liverpool,
Mario Balotelli amesafiri hadi jijini Milan, kufanya vipimo ya afya leo
Jumanne tayari kujiunga na timu yake ya zamani ya AC Milan kwa mkopo kwa
muda mrefu.
Mshambuliaji huyo,
amekuwa akifanya mazoezi peke yake kwa muda wa mwezi sasa, kabla ya
kusafiri hadi Italia kufanya mazungumzo na Sinisa Mihajlovic.
Taarifa ya timu hiyo imesema Mario Balotelli amefika kliniki ya La Madonnina tayari kwa vipimo vya afya.
Kwa mujibu ya makubaliano ya uhamisho huo, klabu ya Liverpool itakuwa ikilipa nusu ya mshahara wa Balotelli akiwa San Siro.
Vilabu vingi vya Ulaya vya Sampdoria, Lazia na Bologna zilionyesha nia
ya kutaka kuhuma ya mchezaji huyu anayesifika kwa ukorofi lakini ni
Milan inayo elekea kupata huduma yake.
Balotelli
amefunga magoli 26 katika michezo 43 akiwa na Milan kabla kuhama timu
hiyo msimu wa (2013 - 2014), huku akicheza mechi 16 akiwa na jezi ya
Liverpool na kufunga goli moja msimu wa (2014 - 2015).
Pia amewahi
kucheza Man City mechi 54 na kufunga magoli 20 msimu wa (2010 -2013), na
Inter Milan mechi tano na magoli mawili kwa misimu ya (2006 - 2010).
Balotelli atakutana na ushindani wa namba klabuni San Siro kutoka kwa Luis Adriano na Carlos Bacca
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni