Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
Baadhi ya vigogo wakiwamo mawaziri, wabunge wameangushwa katika kura za maoni za kutafuta wagombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Miongoni mwa waliangushwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Wamo pia Manaibu mawaziri wa mambo ya ndani ya nchi na mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
ZANZIBAR
Kwa upande wa Zanzibar, Wabunge na wawakilishi wa CCM wanaotetea tena nafasi hizo wengi wamejikuta wakianguka.
Wabunge na wawakilishi hao waliotupwa katika kura hizo yumo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, aliekuwa akigombea ubunge jimbo la Paje wilaya ya Kusini Unguja.
Mahadhi alipata kura 1,785 na dhidi za mshindi, Jafari Sanya Jussa, aliyepata kura 3,368 wakati nafasi ya uwakilishi ikienda kwa Jaku Hashim Ayoub.
Pia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perera Ame Silima, alishindwa kutetea nafasi yake ya ubunge jimbo la Kwamtipura baada ya kuangushwa.
Naye mwanasiasa mkongwe aliyetumikia nafasi ya uwaziri kwa miaka mingi kuanzia awamu ya Muhammed Seif Khatibu mbunge wa jimbo la Uzini amebwagwa kwa kupata kura 1,333 dhidi ya mpinzani wake Salum Mwinyi Rehani alipata kura 1,521.
Vigogo wengine walioangushwa ni Mbunge wa jimbo la Dimani, Abdallah Sheria; Waride Bakari Jabu, mbunge wa jimbo la Kiembe Samaki; Yahya Kassim Mbunge wa Chwakwa; Juma Sururu, Mbunge wa jimbo la Bububu na Amina Andrew, mbunge wa Koani na mwakilishi wa jimbo wameangushwa.
Wamo pia Mwakilishi jimbo la Chaani Ussi Jecha Simai; Mwakilishi wa Kikwajuni, Mahmoud Mussa, Mwakilishi wa jimbo la Mkwajuni, Mbarouk Wadi Mtando na Mwakilishi jimbo la Bubwini, Mlinde Mbarouk.
Wengine ni Nasibu Salum ambaye ni mbunge wa Mfenesini, mbunge wa Tumbatu, mbunge wa Bubwini, mbunge wa jimbo la Fuoni, mwakilishi wa jimbo la Fuoni Thuwaiba Kisasi, mwakilishi wa jimbo la Amani, Fatma Mbarouk; mbunge wa jimbo la Dole, Silvester Mabumba na mwakilishi wa jimbo la Jang’ombe, Suleiman Othman Nyanga.
Baadhi ya wagombea waliopita mi Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi ambaye anawania uwakilishi Mahonda; Shamsi Vuai Nahodha, ubunge jimbo la Kijitoupele; Saada Salum Mkuya, ubunge jimbo la Welezo na Salum Turk ,ubunge jimbo la Mpendae.
Pia Hamad Yussuf Masauni, ubunge jimbo la Kikwajuni; Haji Omar Kheir, uwakilishi jimbo la Tumbatu; Makame Mshimba Mbarouk, ubunge jimbo la Kiwengwa na Haroun Ali Suleiman jimbo la Makunduchi.
Wengine ni Sadifa Juma Khamis ubunge jimbo la Donge; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi anayewania ubunge jimbo la Kwahani na Muhammed Raza, uwakilishi jimbo la Uzini,
Wengine ni Ali Salum, uwakilishi jimbo la Kwahani na Mwakilishi wa Mpendae, Muhammed Said Dimwa.
Hata hivyo baadhi ya majimbo uchaguzi huo wa kura za maoni ilirudiwa jana kutokana na kasoro zilizojitokeza likiwano jimbo la Magomeni.
JIMBO LA NACHINGWEA
Hassan Masalaga alipata kura 494 na kumwangusha waziri Chikawe 128, Amandus Chinguile 127 na Issa Mkalinga 466.
JIMBO LA LUSHOTO
Mbunge anayemali zamuda wake, Henry Shekifu alibwangwa na Shaban Shekilindi.
JIMBO LA MLALO
Waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya tatu, Mbunge wa jimbo hilo, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi. ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kubwagwa na Rashid Shangazi.
IRINGA MJINI
Katika Jimbo la Iringa Mjini lililokuwa na watia nia 13, Fredrick Mwakalebela alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 4,388.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu amepata kura 2,077, Yahaya Msigwa 1,097, Augustine Mahiga 745, Mahamood Madenge 423, Ado Mwasongwe, 259, Nuru Hepautwa 191, Frank Kibiki 183, Maiko Mlowe 183, Fales Kibasa 171, Kiponda Stephan 135, Mwanilwa Joseph 79 na Adelino Gwilino 66.
JIMBO LA KALENGA
Geofrey Mgimwa ametetea nafasi yake kwa kupata kura 15,550.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amepata kura 674, Jackson Kiswaga 3,439, Bryson Kibasa 289, George Mlawa 301.
JIMBO LA ISMANI
Mbunge wa Ismani Willium Lukuvi, ameibuka mshindi kwa kura 10,799, Festo Kiswaga 1237, Hamis Maliga 323, Eliasa Kazikuboma 62, Kiyoyo Antony Sebastian 155. zilizoharibika zilikuwa kura 42.
Katibu wilaya ya Iringa, Elisha Mwampashi, aliwataka wagombea hao kuwa wamoja kwa ajili ya kukijenga chama huku akisema wagombea hao wasiwabeze wenzake ambao kura hazikutosha.
Akizungumza kwa niaba ya wagombea hao, Ado Mwasongwe alisema maendeleo ya Iringa yanajegwa na wana-Iringa wenyewe.
MOSHI MJINI
Mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Davis Mosha, ameibuka msindi wa kura za maoni ya ubunge, jimbo la Moshi Mjini (CCM), baada ya kupata kura 5,271 sawa na asilimia 75, akifuatiwa na Buni Ramole, kura 439.
Mosha, atapimana ubavu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu na mgombea wa (Chadema), ambaye pia ni Meya wa Manispa ya Moshi, Jaffary Michael.
JIMBO LA MOSHI VIJIJINI
Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, ame ibuka kidedea katika kura za maoni za ubunge baada ya kupata kura 5,610 dhidi ya mpinzani wake mkuu, Ansi Mmasy aliyeaokota kura 3,181.
Dk. Chami atakwaana vikali katika uchaguzi mkuu wa mawaka huu na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Lucy Owenya ambaye anapeperusha bendera ya chama hicho.
JIMBO LA HAI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha Danstan Mallya ameshinda kwa kishindo baada ya kupata kura 8,250 na kumbwaga Mjumbe wa Hlamashauri Kuu ya Taifa ya CCM (Nec), Fuya Kimbita aliyeambulia kura 2,275.
Mallya sasa atapambana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ambaye anatetea kiti chake cha ubunge wa jimbo la Hai. Mbowe atasimama kwa niaba ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
JIMBO LA VUNJO
Mwandaaji wa mashindano ya Riadha nchini (Uhuru Marathon), Innocent Meleck ameibuka mshindi wa kura za maoni ya ubunge, jimbo la Vunjo baada ya kupata kura 4,548 dhidi ya kura 1,457 za mpinzani wake, Profesa Mwidadi Mmbaga aliyeambulia kura 1,4,57.
Innocent atakumbana na na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia atakayesimama katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu; kwa niaba ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
SIHA
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, ameshinda kiti cha ubunge, jimbo la Siha baada ya kumbwaga mpinzani wake, Annael Nanyaro kwa kura 12,893 dhidi ya 1,876.
Sasa Mwanri atavaana na mgombea wa Chadema, Dk. Godwin Molell ambaye kabla ya kujiunga upinzani, alikuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara (RMO) na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Siha.
JIMBO LA ROMBO
Kada wa CCM, Colman Samora ameshinda kura za maoni za ubunge jimbo la Rombo, baada ya kupata kura 4,481 dhidi ya mshindani wake Evod Mmanda aliyeambulia kura 1,906.
Samora ndiye atakayechuana na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
SIMANJIRO
Christopher ole Sendeka alikuwa anaongoza katika kata 12 kati ya 16 akifuatiwa na Peter Treima ambaye ameongoza katika kata tatu huku Lenganasa Seipei kata moja.
ARUMERU
Wilaya ya Meru, kwa mujibu wa Katibu wa CCM, Langael Akyoo, wagombea ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, John Palangyo (11,342), Sioi Sumari (3,491), Willium Sarakikya (3,159), Dk. Daniel Palangyo (1,646), Elirehema Kaaya (818), Jel Palangyo (321) na Mhoho Jackson (178),
MONDULI
Katibu wa CCM wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, amentangaza mshindi kuwa ni Namerok Sokoine (29,582). Wagombea wengine ni Kabuti, (155), Amani Amani Torongei (107), Mbayani Tayai (226), Lorinyo Mkoosi kura (238) na Lota Sanare (8,869).
KARATU
Jimbo la Karatu matokeo ya kata 10 kati ya 14, Dk. Wilbard Lory alikuwa mbele (17,711), Rajabu Malewa (911) John Dodo (745) na Joshua Mbwambo, (67).
Kwa mujibu wa Katibu wa Wilaya wa CCM, Loth Ole Lemeirut yakisalia matokeo ya kata nne.
KIGOMA MJINI
Jimbo la Kigoma Mjini, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Warid Kabourou, aliibuka mshindi kwa kura 8,461 na dhidi ya Zuberi Mabiwe (2,740), Elisha Zilikana (1,793) na Sospeter Gabriel (998).
MUHEZA
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajabu, ameibuka mshindi katika kura za maoni kinyang’anyiro cha ubunge Jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza, Mohamed Moyo, alisema jana kuwa Adadi ameshinda kwa kupata kura 7,197 na kufuatiwa na Grace Mtunguja, aliyepata kura 5,033, Allan Mhina (3,816), Mbunge anayemali za muda wake, Hurbert Mntangi (2,502) na Omari Mhando (2,036).
Wengine ni Luick Gugu, aliyepata (1,265), Hassan Bomboko (1,181), Julius Semwaiko (1,102), Nicholaus Mgaya (692), Issa Msumari (624), Mussa Kopwe (545), Hamis Ngoda (302) na Rajabu Nkalange (262).
HANDENI
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda ametangazw kuwa mshindi katika Jimbo la handeni.
BUMBULI
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, wamefanikiwa kutetea nafasi yake ya kuliongioza Jimbo la Bumbuli.
PANGANI
Pangani Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Jumaa Awesso, ali mwangusha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Salehe Pamba.
Katibu wa CCM mkoa wa Tanga Shija Othman aliiambia NIPASHE kuwa mpaka sasa ni majimbo sita tu ambayo matokeo yake yamekamilika huku baadhi ya majimbo ikiwemo lile la Kilindi kulazimika kurudia upigaji kura kutokana na uvumi wa baadhi ya kura kupotea.
KOROGWE MJINI
Mary Chatanda alimbwaga aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Yussuph Nassir.
KOROGWE VIJIJINI
Stephen Ngonyani maarufu kama Professa Maji Marefu, ametetea nafasi yake kwenye Jimbo la Korogwe Vijijini.
TANGA MJINI
Katika Jimbo la Tanga MJINI, Mbunge aliyemaliza muda wake, Omary Nundu, amembwaga Mjumbe wa NEC, Salim Kisauji.
TUNDURU
MENEJA wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Tandahimba na Newala (Tanecu), Daimu Idd Mpakate anaongoza katika matokeo ya awali ya ubunge wa jimbo la Tunduru Kusini lililopo mkoani Ruvuma ndani ya CCM.
Mpakate amepata zaidi ya kura 10,000 katika tarafa za Namasakata, Nalasi na Lukumbule na kumtangulia mbunge anayemaliza muda wake, Alhaji Mtutura Mtutura na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Mtwara, Mwalimu Mtamila Achikuwo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Tunduru, Mohammed Lawa Mpakate, alisema ofisi yake ilikuwa inaendelea kukusanya takwimu za matokeo hayo na kuahidi kutangaza baada ya kukamisha kazi ya kuhesabu.
BUKOBA MJINI
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki, ameshinda baada ya kupata kura 6, 971.
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Bukoba mjini, Ramadhan Kambuga, alisema katika kinyang’anyiro hicho, kilichokuwa na wagombea wanane, Dk. Anatory Amani alipata kura 944 na kufuatiwa na mwalimu George Rubaiyuka (113).
Josephat Kaijage (71), Mujuni Kataraiya (53), Philbert Katabazi (34), Celestina Rwezaura (29) na Elieth Projestus Lukomoka (19).
BABAJI MJINI
Kisyeri Werema Chambiri ameongoza kwa kupata kura 3,722, Ally Msuya (1,758), Janes Dalabe (904), Qwetso Ramadhan (576), Dk. Hindi M Hindi (551), Samo J. Simon (409), Ally Sumaye (357), Cosmas Masauda Bura (283) na Brazza D. Solgati (162).
LUDEWA
Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe, Hosea Mpagike, alimtangaza mbunge wa sasa wa Ludewa anayemaliza muda wake, Deo Filikunjombe, kuwa ameongoza kwa kupata kura 18,290, Zephania Chaula (70) na Jacob Mpangara 205.
NJOMBE MAGHARIBI
Naibu Waziri wa Ujenzi, Grayson Lwenge, ameongoza kwa kura 11,324, Thomas Nyimbo (1,871, Yono Kevela (1,819), Petro John (467), Richard Magenga (417), Abraham Chaula (382) Danford Mpumilwa (332), Hoseana Bumogero (322).
Malumbo Mangula (304), Nepchard Msigwa (216), Abel Bade 106 na Estom Ngilangwa 47.
JIMBO LA MAKAMBAKO
Deo Sanga ameshinda kwa kupata kura 7,643 dhidi ya mpinzani wake Alimwimike Sahi, aliyepata kura 499.
NJOMBE KUSINI
Edward Mwalogo 3,870, Maenda 218, Dioniol Msemwa 1,676, Arnold Mtewele 186, Alfred Luvanda 978, Mwaijinga 86, Hassan Mkwawa 152 na Vitalis Konga 76.
JIMBO LA LUPEMBE
Joram Hongoli kura 2,233, Jeston Kaduma 1,912, Oscar Msigwa 1,656.
KYELA
Dk.Harrison Mwakyembe ameibuka kidedea baada ya kupata kura 15,516 akifuatiwa na George Mwakalinga aliyepata kura 4,900, huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija akiambulia kura 2,301.
Nafasi ya nne ni Asajile Mwambambale 994, Prof.Mwaikambo Yesaya alipata kura 283, Gabriel Mwaipopo (785, Jackison Mwakapiso (601, Fire Mwamakimbula 881, John Mwambembwa 263 na Richard Mwikasyege alipata kura 442.
JIMBO LA MBOZI
Godfrey Zambi ametetea nafasi yake baada ya kpata kura 11,286 akifuatiwa na George Mwanisongole aliyepata kura 4,558 huku Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 2,956.
JIMBO LA VWAWA
Japhet Hasunga ameshinda kwa kupata kura 10,902, Mchungaji Tito Nduka alipata kura 3,911 na Dismas Haonga kura 2,205.
JIMBO LA RUNGWE
Richard Kasesela ameongoza kwa kupata kura 8,596 akifuatiwa na mfanyabiashara Amon Sauli aliyepata kura 8,562 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Akim Mwambene kura 2,569.
JIMBO LA KILOSA
Mbaraka Bawazir 6,742, Ameir Mbaraka 3,570 na Zuhura Lilola kura 1,682.
JIMBO LA MIKUMI
Jonas Nkya kura 947, Omar Kiputiputi 604 na Abdusalaam Amer kura 544.
MOROGORO MJINI
Abdulaziz Abood 20,094 na Simon Berege kura 429.
JIMBO LA MLIMBA
Godwin Kunambi 6,233, Frederick Sagamiko 2,203 na Jane Mihanji kura 2,073.
JIMBO LA KILOMBERO
Abubakari Asenga 9,629, Abdallah Lyana 3,999 na Abdul Mteketa alipata kura 2,646.
JIMBO LA ULANGA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani 12,035, Agustino Matefu 2,736 na Kitolero Daudi kura 194.
MVOMERO
Katika Jimbo la Mvomero Sadiq Murad alikuwa anaongoza katika kata 21 dhidi ya kata tisa dhidi ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala katika matokeo ya awali.
MTAMA
Mshindi jimbo la Mtama Nape Nnauye amepata kura 9,347 akifuatiwa na Seleiman Luwongo aliyepata kura 4,766 na Janety Nayenga 850.
MCHINGA
Jimbo la Mchinga, mshindi ni Said Mtanda kura 3,100, Megu Yusuph kura 1,821 na Riziki Ulida 2,217.
LINDI MJINI
Lindi Mjini aliyeshika nafasi ya kwanza ni Hassan Kaunje kura 3,428, Mohammed Utali kura, 2,314 na Hassan Jaruf kura 1,595.
MKURANGA
Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani, matokeo ya awali yanaonyesha, Abdala Ulega anaongoza kwa kupata kura 11,008 akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Kighoma Malima kura 6,008.
Hata hivyo halisi mpaka jana jioni yalikuwa hayajapatikana ingawa inaelezwa kuwa, Malima alikuwa amezidiwa katika kinyang’anyiro hicho.
NEWALA MJINI
George Mkuchika kura 5,826, Rajab Kazibure kura 3,247, Kwame Daffari kura 1,617.
MTWARA VIJIJINI
Hawa Abdulrahman Ghasia, alipita bila kupingwa.
NANYUMBU
Abdallah Chikota kura 12,388, Swalehe Livanga kura 2,376.
MASASI
Mkata Cleverland Joseph kura 100, Mande Mathew Mike 186, Frank Edwin Ekoni 353, Mnonjela Victor Joshua 441, Kombani Zaburi Regnald 533, Mtaki Zomari Magreth 1,386, Mwambe Edfonce Jofrey 1,787, Chua Chua Mohamed Rashid 2,412
JIMBO LA LULINDI
Halinga Richard Enock kura 896, Sowani Gabriel Thomas 1,048, Bwanausi Dismus Jerome 11,745
NDANDA
Mrope Alfonce Regnald 863, Mwambe David Cecil 4,951, Mariam Reuben Kasembe 5,453
JIMBO LA MTWARA MJINI
Hussein Bakari Kasugulu 791, Said Mussa Swala 393, Mussa Mohamed Chimae 217, Hasnein Mohamed Murji 10,055 Salum Abilah Nahodha 114.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shaibu Akwilombe, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara.
Imeandikwa na Godfrey Mushi, Kilimanjaro; Cynthia Mwilolezi, Arusha; Lulu George na Stephen William, Tanga; Stevie Chindiye, Tunduru; Lilian Lugakingira, Bukoba; Furaha Eliab, Njombe; Friday Simbaya, George Tarimo, Iringa; rahma Suleiman, Zanzibar, Thobias Mwanakatwe, Dar; Ashton Balaigwa, Morogoro; Lucy Ogiti Lindi, Yasmin Protas, Pwani na Juma Mohamed, Mtwara.
chanzo; nipashe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni