Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya
Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba
ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Dkt
Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya
kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu
wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.
Magufuli
ambaye yupo katika mikoa ya Nyanda za juu kusini katika kampeni ya
kusaka nafasi ya kuwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema
suala la afya litakuwa moja ya ajenda zake muhimu atakapoingia
madarakani.
Katika
hatua nyingine Dkt Magufuli amewaleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa
ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya
Mafisadi na Wala rushwa.
Mbunge
wa zamani wa jimbo la Kyela Mzee John Mwakipesile akimpigia debe
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli wakati mgombea huyo alipofika
jimboni humo kuomba kura za wananchi ili wamchague kuwa rais.Mzee
Mwakipesile amesema kuwa anamuunga mkono Dkt Magufuli na atahakikisha
anashiriki kikamilifu kuhakikisha mgombea huyo anaibuka na ushindi kwa
kishindo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akimpigia debe Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika
viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jionu ya leo.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano wa kampeni
uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu
aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza
Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.
Maelfu
ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nzovwe Mbeya
jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia
wananchi hao.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano wa
kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo
Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za
ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze
kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za
kuongoza nchi.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya
Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba
ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano,Magufuli amewaambia
wananchi hao kuwa atahakikisha huduma za afya zinaimarishwa
ipasavyo,katika suala la Elimu Magufu aliwaeleza Wananchi kuwa iwapo
watamchagua katika nafasi hiyo ya Urais atahakikisha elimu kuanzia
darasa la kwanza mpaka kidato cha nne itatolewa bure,aidha pia amewataka
Watanzania kuwa wamoja katika kuhakikisha wanailinda na kuitunza amani
iliyopo nchini.
Wananchi
wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa
akiwahutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Nzovwe mjini
Mbeya.
Maelfu ya
Wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya
wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo.
Karibu tena katika blogs hii kwa habari mbali mbali ;THOMAS WIKESI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni