TANGAZO

TANGAZO

Jumatano, 30 Desemba 2015

SABABU 5 KWANINI MESUT OZIL NI KIPAJI ADIMU

mesut-ozil-arsenal_3010111.jpg

Tangu atue Arsenal misimu miwili iliyopita kwa ada ya pauni milioni 42 kutoka Real Madrid mchezaji Mesut Özil, klabu yake ya Arsenal imekua hailali njaa.

Wametwaa makombe ya chama cha soka FA cup katika misimu hii miwili mfululizo, Ozil akiwa chachu ya mafanikio hayo. Msimu huu pia Arsenal wako kileleni hadi sasa na tayari Mesut Ozil anakaribia kuvunja rekodi ya kutoa pasi nyingi za magoli (assists) hadi sasa ana assists 16, si kitu cha kawaida.

WAZIRI MAGHEMBE ATEMA CHECHE.......ASEMA WALIOMUITA 'WAZIRI MZIGO' WATAISOMA NAMBA



Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, aliyeapishwa jana kushika wadhifa huo na Rais Dk. John Magufuli, amefunguka na kueleza sababu za kuitwa Waziri ‘mzigo’ wakati akiwa Wizara ya Maji, akitokea Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

KUMBE HII NDIYO HISTORIA YA MKALI BONGO MOVIE WEMA SEPETU?ISOME YOTE UMJUE VIZURI


Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28, September, ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa Mzee Sepetu.

Wema hakufikiria kama atakuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa nchini hadi nchi za nje mpaka siku mmoja alipo kuwa kwenye matembezi yake Slypway Masaki alikutana na dada Mange Kimambi na kushawishiwa ashiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006...

SAMATTA: NGUVU YA MASHABIKI ILINIFANYA NISAJILIWE TP MAZEMBE

Rais wa TP Mazembe Moise Katumbi (katikati) akiwa kazungukwa na kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo

Rais wa TP Mazembe Moise Katumbi (katikati) akiwa kazungukwa na kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo
Tunaendelea na ‘Safari Ndefu ya Mbwana Samatta kutoka Mbagala kwenda Ulaya’ jana tuliangalia namna ambavyo Samatta alitoka African Lyon akajiunga na wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na maisha yake yote akiwa Simba. Leo tunaangalia namna alivyojiunga na timu ya TP Mazembe ambayo ndiyo imemtambulisha kwenye soka la Afrika na duniani.
Samatta anasema nguvu ya mashabiki ndiyo iltumika kumsajili yeye na haikuwa pendekezo la mwalimu wala rais wa timu hiyo

DJ wa Jay Z katua Dar es Salaam.. kumbe ana washkaji TZ !! Mengine kwenye dakika 3.. +Video


Jamaa anaitwa DJ Young Guru, huyu ndio jamaa ambae anafanya kazi kama DJ wa rapper Jay Z akiwa kwenye show zake… Hii ni safari ya pili kwa Young Guru kukanyaga Tanzania.

Pichaz 7 za Mbwana Samatta alivyokutana na waziri wa michezo Nape Nnauye wizarani Dec 30 …


December 30 ilikuwa ni siku ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta kukutana na uongozi wa wizara ya habari, vijana, utamaduni, burudani na michezo Nape Nnauye

Waziri akuta ‘ofisi nzima’ wako likizo

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula      


Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amefanya ziara ya kushtukiza Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukuta zaidi ya nusu ya watendaji wake wako likizo.
Naibu Waziri huyo aliwasili ofisini hapo jana saa 8.30 mchana na kupokewa na mtunza kumbukumbu, Bahati Kassim ambaye ni mtumishi pekee aliyekuwapo ofisini.

Jumanne, 29 Desemba 2015

Serikali kuwabana madaktari inaowasomesha nje ya nchi

Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo yaNaibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla

Shinyanga. Serikali imesema madaktari wote watakaopata nafasi ya kusoma nje ya nchi kwa ufadhili wake, watafanya hivyo kwa kusaini mkataba.
Kufanya hivyo kumeelezewa kuwa kutasaidia kuwabana wale wanaohitimu na kutimkia nje ya nchi kwenda kufanya kazi huko.

Kipindupindu chashika kasi Nyamagana, Magu

Mwanza. Ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kuzitesa Wilaya za Nyamagana na Magu mkoani hapa, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka na kufikia 17, huku mtu mmoja akipoteza maisha wilayani Magu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa, Dk Rwekyendela Onesmo alisema licha ya jitihada zinazofanywa, ugonjwa huo unazidi kuzikumba baadhi ya wilaya za mkoa huo.
“Kwa sasa tunao jumla ya wagonjwa 17 kati yao Nyamagana na Magu wapo wanane kwa kila wilaya na Ilemela yupo mgonjwa mmoja kwa sasa,” alisema.

Mkubwa Fella kwenye headlines za utambulisho wa kundi jipya Salamu TMK…(Video)


Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Said Fella time hii anakualika kuangalia video ya vijana wake wapya wapo saba ambao wanaunda kundi jipya lililopewa jina la Salamu TMK.
Vijana hao wameachia video ya single yao mpya ya

Ubelgiji yanasa ‘waliopanga’ shambulio Mwaka Mpya

 Ubelgiji

Polisi nchini Ubelgiji wamewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kupanga mashambulio mkesha wa siku ya Mwaka Mpya mjini Brussels.
Walikamatwa kwenye misako ya polisi Jumapili na Jumatatu mjini Brussels na katika mikoa ya Flemish Brabant na Liege.

Rais mpya wa Burkina Faso kuapishwa leo


Aliyekuwa waziri mkuu wa Burkina Faso Roch Mark Christian Kabore, anaapishwa leo kama rais nchi hiyo .
Bwana Kabore ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita, alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani Blaise Compaore, ambaye alinyakua mamlaka baada ya mapinduzi ya jeshi, na kutawala taifa hilo kwa miaka 27 hadi mapinduzi ya umma mwaka uliopita.
Kabore alitofautiana na Compaore mwaka uliopita alipotangaza nia ya kuendelea kuongoza.

Waasi wa SPLM: Tumeua wanajeshi 13 wa Sudan


Waasi wa SPLM: Tumeua wanajeshi 13 wa Sudan
Waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini (SPLM-N) wamedai kuwa wameua askari 13 wa jeshi la nchi hiyo, katika jimbo la Blue Nile.
Msemaji wa harakati hiyo Arno Nugutlu Lodi amesema kuwa hadi sasa wameshaua wanajeshi 13 wa serikali ya Sudan na kuzima hujuma zao katika eneo la Torda, kaunti ya Bau katika jimbo la Blue Nile.
Amesema walifanikiwa kuzima uvamizi wa jeshi la Sudan katika mapigano yaliyojiri kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 7 adhuhuri Jumamosi iliyopita.

Waasi wa Rwanda wapigana na Maimai nchini DRC


Waasi wa Rwanda wapigana na Maimai nchini DRC
Kumezuka mapigano baina ya waasi wa Rwanda na Maimai mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano hayo.
Shirika la habari la Xinhua limeripoti habari hiyo na kuzinukuu duru za ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikisema kuwa, watu saba wameuawa katika mapigano baina ya waasi wa Rwanda wa FDLR na wale wa Maimai wa UPDI mkoani Kivu Kaskazini.

SASA RASMI, SIMBA YATANGAZA KUANZA KUJENGA UWANJA WAKE WA MAZOEZI

     
Uongozi wa Simba umesema utaanza rasmi kujenga uwanja wao wa mazoezi mwezi ujao.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watautumia uwanja wao wanaoumiliki kuanza kujenga uwanja wa mazoezi.

MINGANGE KUYATUMIA MAPUMZIKO VIZURI KUIPA NGUVU MBEYA CITY



Kocha wa Mbeya City, Abdul Mingange amesema atatumia muda wa mapumziko kujipanga upya kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

GUARDIOLA ATUA KENYA KWA AJILI YA MAPUMZIKO

 

 

Kocha huyo ametua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa JKIA akiwa na mkewe Cristina Serra na watoto wake Maria, Marius na Valentina Guardiola.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona, alipiga picha na baadhi ya mashabiki akiwemo Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU, MKOANI KIGOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa zawadi ya khanga,blanket na ndoo kwenye wodi ya wazazi katika zahanati iliyopo kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa Mama mkimbizi kutoka nchi ya Burundi aliyejifungua.

Sheria za ardhi kikwazo kwa wakulima

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Morogoro. Wakulima wadogo wilayani Kilosa wameonekana kukosa ufahamu wa sheria za ardhi, jambo linalowafanya kushindwa kufuatilia kwa makini masuala ya ardhi pale inapotokea migogoro katika maeneo yao.
Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Miradi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Adam Nyaruhuma alisema hayo katika mkutano wa wakulima wadogo wilayani humo, juu ya utafiti kuhusu migogoro ya ardhi alioufanya na kugundua upungufu uliopo.

Ufisadi mwingine waibuliwa bandarini Dar

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Serikali imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.

RAIS MAGUFULI AZIDI KUTIKISA VIGOGO.JIPU LA MADAWA YA KULEVYA LAANZA KUTUMBULIWA,VIGOGO WAANZA KUKAMATWA WENGINE MATUMBO JOTO


  WALE vigogo wanaosadikiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ‘unga’ nchini wameanza ‘kutumbuliwa majipu’ kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuanza kuwakamata.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo, vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo walikamatwa wiki iliyopita katika maeneo ya Kinondoni, Ilala na Temeke, Dar baada ya wengine wengi kukamatwa siku za nyuma kutokana na kudaiwa kuingiza unga nchini kwa nyakati tofauti.

HIVI NDIVYO SAMATA ALIVYO PATA NAMBA YA KUDUMU SIMBA

Mbwana Samatta 2
Hakuna ubishi kwamba kila mafanikio yanakuja kwa bidii, kujituma, kujitoa, nidhamu na vitu vingine vingi sana tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria kwamba unaweza ukapata mafanikio kwa njia ya mkato bila kupambana.
Mafanikio aliyonayo leo Super Star wa soka la Bongo Mbwana Samatta hayajaja hivihivi ‘kimagumashi’, jamaa alikuwa anatoka nyumbani saa 10:30 alfajiri ili awahi mazoezi ambayo ylikuwa yanaanza saa 1:00 asubuhi.

PETR CECH AMEWEKA REKODI MPYA YA KUKUMBUKWA EPL

Cech

Petr Cech amevunja rasmi rekodi ya kuwa kipa aliyecheza mechi nyingi bila ya kufungwa ‘clean sheets’ katika historia ya Ligi Kuu Engalnd.
Cech, 33,  amevunja rekodi ya David James baada ya kufikisha idadi ya ‘clean sheets’ 170 katika mchezo wa jana usiku dhidi ya Bournemouth ambapo Arsenal walishinda kwa magoli 2-0.

Serikali yashtukia vifaa tiba asili, mbadala


Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kutotambuliwa kwa mkutano wa waganga wa tiba mbadala uliofanyika juzi.
PICHA NA :MWANANCHI COMMUNICATION.

Dar es Salaam. Serikali imesema ina taarifa za kuingizwa kwa mashine za kuchukulia vipimo bila ya kusajiliwa na kusisitiza kuwa itaweka bayana msimamo wake baada ya siku 14 ilizotoa kwa matabibu wa tiba mbadala kuwasilisha taarifa za huduma zao.

Ahadi ya JPM ya ujenzi wa reli kuanza



Rais John Magufuli  

 

Kigoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanza ziara mkoani Kigoma huku akiahidi kuanza ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya viwango vya ‘standard gauge’, itakayosaidia kuimarisha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kupitia Bandari ya Kigoma.
Tamko la Waziri Mkuu Majaliwa inaashiria kuanza kwa utekelezaji wa vipaumbele 25, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati, alivyovitoa Rais John Magufuli (wakati huo akiwa mgombea urais wa CCM), Agosti 24, wakati wa uzinduzi wa kampeni zake kwenye Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam.

Mahakama yatupa pingamizi la ubunge dhidi ya Dk Mwakyembe

Waliokuwa wagombea ubunge, Jimbo la Vwawa,
 Waliokuwa wagombea ubunge, Jimbo la Vwawa, Fanuel Mkisi (wa pili kutoka kulia) na John Mwambigija (wa pili kushoto) wa jimbo la Rungwe, wote wa Chadema, wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya jana wakisubiri kusikiliza kesi zao walizofungua za kupinga matokeo yaliyowapa ushindi wagombea wa CCM katika majimbo hayo.

 Mbeya. Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, imetupilia mbali shauri la kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe(CCM).
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema, Abraham Mwanyamaki baada ya kushindwa kulipa Sh3 milioni ambazo ni dhamana ya kesi kwa anaowalalamikia.

Wanafunzi 70 wapoteza mwelekeo wa shule baada ya bomoabomoa Dar


PICHA:MWANANCHI

Dar es Salaam. Zaidi ya wanafunzi 70 wa shule za msingi na sekondari huenda wakashindwa kuendelea na masomo, baada ya familia zao kukumbwa na bomoabomoa kwenye Bonde la Mto Msimbazi, na kukosa mahali pa kushi.
Zimeshapita siku 12 tangu zaidi ya nyumba 300, zilizojengwa kwenye bonde hilo zibomolewe na kulazimisha wakazi kuhamia sehemu nyingine na baadhi kuishi juu ya vifusi.

Jumanne, 22 Desemba 2015

RAIS KAGAME AMPONGEZA MAGUFULI

Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji. Rwanda, ambayo haijapakana na bahari, imekuwa ikiitegemea Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo yake. Rais Kagame, ambaye miaka miwili ilkiyopita aliwahi kukosoa waziwazi utendaji wa Bandari akieleza kuwa angepewa taasisi hiyo angeweza kukusanya mapato ambayo yangeiendesha Tanzania, sasa anaonekana kuridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano za kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi kwenye bandari hiyo kongwe. Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari. Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo. Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda. Mapema mwezi huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kushughulikia matatizo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Pia, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe na kuagiza uchunguzi dhidi yao uanze mara moja, alivunja Bodi ya Wakurugenzi TPA. Kushirikiana na ADB Katika hatua nyingine, Rais amemhakikishia mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na kumhakikishia ushirikiano, Rais ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa. Kwa upande wake, Dk Kandiero alisema benki hiyo iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga Dola 2.3 bilioni kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Alisema ADB imelenga kujielekeza kutoa mikopo katika sekta ya nishati na usafiri.

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
            Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu

Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji.

Jumatatu, 21 Desemba 2015

Huyu ndiie Henricko (hk) ambae amepanga kufanya hiki katika mziki wake sikiliza na kudownload hapa

Msanii huyu ambae alivuma na kibao cha Wajanja ambae ni Henricko (hk) hivi sasa amepanga kufanya ngoma  kali ya kufungia mwaka baada ya kutoa ngoma hii mpya  alioifanya kwa C1 studio yaG.time na sasa kama bado

KINGWENDU ASEMA HIKI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Image result for PICHA KINGWENDU
Msanii wa vichekesho maarufu kama Kingwendu amewasihi vijana ambao wanatumia Madawa ya kulevya waachane nayo kwani ya naathali kubwa sana katika maisha ya binadamu,

Akizungumza na Thomas wikesi blogs Kingwendu amesema kuwa yeye anakuwa msitari wa mbele kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya .

Jumamosi, 12 Desemba 2015

Picha 3 za show ya Yamoto BAND Washington DC Marekani



Yamoto Band walisafiri kwenda Marekani kwa ajili ya shows kwenye miji mbalimbali na kukutana na Watanzania waishio Marekani ambao kwa kiasi kikubwa wamekua na kiu ya kuwaona kwenye stage Yamoto ambao ndio mara yao ya kwanza Marekani na hizi picha kwenye hii post ni za show yao ya Washington DC.

Mwakyembe Aomba Apewe Muda......Azungumzia Katiba Mpya

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ameapishwa leo na rais John Magufuli kushika wadhifa huo amewaomba wadau na wananchi kwa ujumla kumpa muda.

Lowassa: Nilishinda Urais Lakini CCM Wakaupora Ushindi Wangu na Dunia Nzima Inajua



Aliyekua mgombea Urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameendelea kudai ndiye mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na dunia inajua.

Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

KINANA AMVAA LOWASA ARUSHA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahmani Kinana akihutubia mkutano wa hadhara.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

TOURE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA BBC BARANI AFRIKA...................



Yaya
Yaya Toure ndiye mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka 2015.
Kiungo huyo wa kati wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 32 anakuwa wa tatu, baada ya Wanigeria

ROONEY ATAKIWA CHINA KWA GHARAMA KUBWA HAIJAWAHI KUTOKEA...........




   
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amepewa ya Pauni Milioni 75 kwenda kuungana na kocha Sven Goran Eriksson nchini China.

Jumanne, 8 Desemba 2015

HAYA SASA, HIZI NI ZILE TOP 5 STORIES ZA USAJILI WA DIRISHA DOGO ZINAZOTIKISA ULAYA

top 5


Dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya Ulaya litafunguliwa mwezi January ili kuvipa fursa baadhi ya vilabu kufanya usajili wa wachezaji kuimarisha vikosi vyao katika ligi mbalimbali ili kutafuta mafanikio au kufanya vizuri kwenye ligi hizo.
Kuna wachezaji na makocha mbalimbali wamekuwa wakitajwa au kuhusihwa na usajili huo unaosubiriwa na wadau wa soka kuona timu wanazozi-support zitafanya nini muda huo ukifika.
Hii hapa top 5 ya majina ya wachezaji na makocha yanayotajwa sana kwa sasa yakihusishwa kujiunga au kutemwa na baadhi ya

SCHWEINSTEIGER ATUPWA JELA YA FA

FA-Rungu 1
Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger 31, anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na chama cha soka England (FA) kutokana na kitendo chake cha kumpiga kiwiko usoni mlinzi wa Westham United, Winston Reid katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana Jumamosi iliyopita.
Schweinsteiger ana hadi Alhamis hii, saa sita mchana kukubali/kukataa kosa hilo baada ya FA kumuadhibu Jumatatu hii. Refarii Marc Clatternburg aliwaita wachezaji wote wawili na kuongea nao, huku asichukue hatua nyingine yeyote kutokana na kutoona tukio hilo.

PLUIJM HATAKI MCHEZO, AMPIGA CHINI MDOGOAKE MSUVA

Simon Msuva akamlisha keki  mdogowake James Msuva (kulia) siku aliyokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) December 3, 2015
Simon Msuva akamlisha keki mdogoake James Msuva (kulia) siku aliyokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) December 3, 2015
Kama ulikua hujui sasa nakufanya ujue kuwa kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm hataki kabisa mchezo linapokuja suala la kazi, hii imemkuta kiungo wa timu hiyo James Msuva ambaye ni mdogo wa Simon Msuva baada ya kuachwa na kocha huyo wakati kikosi cha Yanga kikiingia kambini kujiandaa na mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Hizi ni rekodi za Messi ambazo hazijawahi vunjwa na mchezaji yoyote



Lionel Messi ni staa wa soka wa kimataifa wa Argentina ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania aliyojiunga nayo mwaka 2001 na mwaka 2003 akaanza kuichezea FC Barcelona C. Lionel Messi anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji soka wenye rekodi za kusisimua zaidi duniani. Hizi ni rekodi 5 za kusisimua za Lionel Messi stori kutoka sokkaa.com
5- Lionel Messi sio tu anatajwa kuwa mchezaji bora wa Dunia, ila wachambuzi wa masuala ya soka wanamuita ni moja kati ya wachezaji bora wa soka waliowahi kutokea katika historia ya soka. Messi ndio mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mara 4, kwani hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo.

Wasanii mbalimbali kutekeleza agizo la Rais MAGUFULI tarehe 9 December…..


Ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa awamo ya tano Dk.John Magufuli kutoa tamko la hakutakua na sherehe za kitaifa December 9 na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.
Sasa time hii headlines za usafi zimewagusa wasanii na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda ambapo tarehe 9 December wataungana kuhakikisha

Jumatatu, 7 Desemba 2015

Moto wa Rais Magufuli umeendelea bandarini, wengine wamesimamishwa leo..

Mpaka leo hii December 07 2015 tunahesabu kama mwezi mmoja hivi umepita tangu RaisMagufuli aapishwe na aanze kazi ya Urais wa awamu ya tano Tanzania.
Mfululizo wa stori zenye uzito wa kasi yake kwenye Urais zimekuwa zikitufikia kila siku, ya leo bado inabeba headlines za bandarini kwa mara nyingine… tangu siku ya kwanza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amefanya ziara ya ghafla bandarini mengi yameripotiwa ikiwemo ishu ya ubadhirifu