TANGAZO
Jumatano, 30 Desemba 2015
WAZIRI MAGHEMBE ATEMA CHECHE.......ASEMA WALIOMUITA 'WAZIRI MZIGO' WATAISOMA NAMBA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa
Jumanne Maghembe, aliyeapishwa jana kushika wadhifa huo na Rais Dk. John
Magufuli, amefunguka na kueleza sababu za kuitwa Waziri ‘mzigo’ wakati
akiwa Wizara ya Maji, akitokea Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
KUMBE HII NDIYO HISTORIA YA MKALI BONGO MOVIE WEMA SEPETU?ISOME YOTE UMJUE VIZURI
Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28, September, ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa Mzee Sepetu.
Wema hakufikiria kama atakuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa
nchini hadi nchi za nje mpaka siku mmoja alipo kuwa kwenye matembezi
yake Slypway Masaki alikutana na dada Mange Kimambi na kushawishiwa
ashiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006...
SAMATTA: NGUVU YA MASHABIKI ILINIFANYA NISAJILIWE TP MAZEMBE
Tunaendelea na ‘Safari Ndefu ya Mbwana Samatta kutoka Mbagala kwenda Ulaya’ jana tuliangalia namna ambavyo Samatta alitoka African Lyon akajiunga na wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na maisha yake yote akiwa Simba. Leo tunaangalia namna alivyojiunga na timu ya TP Mazembe ambayo ndiyo imemtambulisha kwenye soka la Afrika na duniani.
Samatta anasema nguvu ya mashabiki ndiyo iltumika kumsajili yeye na haikuwa pendekezo la mwalimu wala rais wa timu hiyo
DJ wa Jay Z katua Dar es Salaam.. kumbe ana washkaji TZ !! Mengine kwenye dakika 3.. +Video
Jamaa anaitwa DJ Young Guru, huyu ndio jamaa ambae anafanya kazi kama DJ wa rapper Jay Z akiwa kwenye show zake… Hii ni safari ya pili kwa Young Guru kukanyaga Tanzania.
Pichaz 7 za Mbwana Samatta alivyokutana na waziri wa michezo Nape Nnauye wizarani Dec 30 …
December 30 ilikuwa ni siku ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta kukutana na uongozi wa wizara ya habari, vijana, utamaduni, burudani na michezo Nape Nnauye
Waziri akuta ‘ofisi nzima’ wako likizo
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
Dar
es Salaam. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Angelina Mabula amefanya ziara ya kushtukiza Ofisi za Baraza la Ardhi na
Nyumba za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukuta zaidi ya
nusu ya watendaji wake wako likizo.
Naibu
Waziri huyo aliwasili ofisini hapo jana saa 8.30 mchana na kupokewa na
mtunza kumbukumbu, Bahati Kassim ambaye ni mtumishi pekee aliyekuwapo
ofisini.
Jumanne, 29 Desemba 2015
Serikali kuwabana madaktari inaowasomesha nje ya nchi
Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla
Shinyanga.
Serikali imesema madaktari wote watakaopata nafasi ya kusoma nje ya
nchi kwa ufadhili wake, watafanya hivyo kwa kusaini mkataba.
Kufanya hivyo kumeelezewa kuwa kutasaidia kuwabana wale wanaohitimu na kutimkia nje ya nchi kwenda kufanya kazi huko.
Kipindupindu chashika kasi Nyamagana, Magu
Mwanza.
Ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kuzitesa Wilaya za Nyamagana na Magu
mkoani hapa, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka na kufikia 17, huku
mtu mmoja akipoteza maisha wilayani Magu.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa, Dk Rwekyendela Onesmo
alisema licha ya jitihada zinazofanywa, ugonjwa huo unazidi kuzikumba
baadhi ya wilaya za mkoa huo.
“Kwa
sasa tunao jumla ya wagonjwa 17 kati yao Nyamagana na Magu wapo wanane
kwa kila wilaya na Ilemela yupo mgonjwa mmoja kwa sasa,” alisema.
Mkubwa Fella kwenye headlines za utambulisho wa kundi jipya Salamu TMK…(Video)
Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Said Fella time hii anakualika kuangalia video ya vijana wake wapya wapo saba ambao wanaunda kundi jipya lililopewa jina la Salamu TMK.
Vijana hao wameachia video ya single yao mpya ya
Ubelgiji yanasa ‘waliopanga’ shambulio Mwaka Mpya
Polisi nchini Ubelgiji wamewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kupanga mashambulio mkesha wa siku ya Mwaka Mpya mjini Brussels.
Walikamatwa kwenye misako ya polisi Jumapili na Jumatatu mjini Brussels na katika mikoa ya Flemish Brabant na Liege.Rais mpya wa Burkina Faso kuapishwa leo
Aliyekuwa waziri mkuu wa Burkina Faso Roch Mark Christian Kabore, anaapishwa leo kama rais nchi hiyo .
Bwana
Kabore ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita, alikuwa mshirika wa
karibu wa rais wa zamani Blaise Compaore, ambaye alinyakua mamlaka
baada ya mapinduzi ya jeshi, na kutawala taifa hilo kwa miaka 27 hadi
mapinduzi ya umma mwaka uliopita.Kabore alitofautiana na Compaore mwaka uliopita alipotangaza nia ya kuendelea kuongoza.
Waasi wa SPLM: Tumeua wanajeshi 13 wa Sudan
Waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini (SPLM-N)
wamedai kuwa wameua askari 13 wa jeshi la nchi hiyo, katika jimbo la
Blue Nile.
Msemaji wa harakati hiyo Arno Nugutlu Lodi amesema kuwa hadi sasa
wameshaua wanajeshi 13 wa serikali ya Sudan na kuzima hujuma zao katika
eneo la Torda, kaunti ya Bau katika jimbo la Blue Nile.
Amesema walifanikiwa kuzima uvamizi wa jeshi la Sudan katika mapigano yaliyojiri kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 7 adhuhuri Jumamosi iliyopita.
Amesema walifanikiwa kuzima uvamizi wa jeshi la Sudan katika mapigano yaliyojiri kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 7 adhuhuri Jumamosi iliyopita.
Waasi wa Rwanda wapigana na Maimai nchini DRC
Kumezuka mapigano baina ya waasi wa Rwanda na Maimai mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa
kwenye mapigano hayo.
Shirika la habari la Xinhua limeripoti habari hiyo na kuzinukuu duru
za ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikisema kuwa, watu saba
wameuawa katika mapigano baina ya waasi wa Rwanda wa FDLR na wale wa
Maimai wa UPDI mkoani Kivu Kaskazini.SASA RASMI, SIMBA YATANGAZA KUANZA KUJENGA UWANJA WAKE WA MAZOEZI
Uongozi wa Simba umesema utaanza rasmi kujenga uwanja wao wa mazoezi mwezi ujao.
Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watautumia uwanja wao wanaoumiliki kuanza kujenga uwanja wa mazoezi.
MINGANGE KUYATUMIA MAPUMZIKO VIZURI KUIPA NGUVU MBEYA CITY
Kocha
wa Mbeya City, Abdul Mingange amesema atatumia muda wa mapumziko
kujipanga upya kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.
GUARDIOLA ATUA KENYA KWA AJILI YA MAPUMZIKO
Kocha
huyo ametua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa JKIA akiwa na mkewe Cristina
Serra na watoto wake Maria, Marius na Valentina Guardiola.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona, alipiga picha na baadhi ya mashabiki akiwemo Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.
WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU, MKOANI KIGOMA
Sheria za ardhi kikwazo kwa wakulima
Morogoro.
Wakulima wadogo wilayani Kilosa wameonekana kukosa ufahamu wa sheria za
ardhi, jambo linalowafanya kushindwa kufuatilia kwa makini masuala ya
ardhi pale inapotokea migogoro katika maeneo yao.
Mkuu
wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Miradi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Dk Adam Nyaruhuma alisema hayo katika mkutano wa
wakulima wadogo wilayani humo, juu ya utafiti kuhusu migogoro ya ardhi
alioufanya na kugundua upungufu uliopo.
Ufisadi mwingine waibuliwa bandarini Dar
Serikali
imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari
2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata
hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na
Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa
mapato.
RAIS MAGUFULI AZIDI KUTIKISA VIGOGO.JIPU LA MADAWA YA KULEVYA LAANZA KUTUMBULIWA,VIGOGO WAANZA KUKAMATWA WENGINE MATUMBO JOTO
WALE vigogo wanaosadikiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ‘unga’ nchini wameanza ‘kutumbuliwa majipu’ kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuanza kuwakamata.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo, vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo walikamatwa wiki iliyopita katika maeneo ya Kinondoni, Ilala na Temeke, Dar baada ya wengine wengi kukamatwa siku za nyuma kutokana na kudaiwa kuingiza unga nchini kwa nyakati tofauti.
HIVI NDIVYO SAMATA ALIVYO PATA NAMBA YA KUDUMU SIMBA
Hakuna ubishi kwamba kila mafanikio yanakuja kwa bidii, kujituma, kujitoa, nidhamu na vitu vingine vingi sana tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria kwamba unaweza ukapata mafanikio kwa njia ya mkato bila kupambana.
Mafanikio aliyonayo leo Super Star wa soka la Bongo Mbwana Samatta hayajaja hivihivi ‘kimagumashi’, jamaa alikuwa anatoka nyumbani saa 10:30 alfajiri ili awahi mazoezi ambayo ylikuwa yanaanza saa 1:00 asubuhi.
PETR CECH AMEWEKA REKODI MPYA YA KUKUMBUKWA EPL
Petr Cech amevunja rasmi rekodi ya kuwa kipa aliyecheza mechi nyingi bila ya kufungwa ‘clean sheets’ katika historia ya Ligi Kuu Engalnd.
Cech, 33, amevunja rekodi ya David James baada ya kufikisha idadi ya ‘clean sheets’ 170 katika mchezo wa jana usiku dhidi ya Bournemouth ambapo Arsenal walishinda kwa magoli 2-0.
Serikali yashtukia vifaa tiba asili, mbadala
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kutotambuliwa kwa mkutano wa waganga wa tiba mbadala uliofanyika juzi.
PICHA NA :MWANANCHI COMMUNICATION.
Dar
es Salaam. Serikali imesema ina taarifa za kuingizwa kwa mashine za
kuchukulia vipimo bila ya kusajiliwa na kusisitiza kuwa itaweka bayana
msimamo wake baada ya siku 14 ilizotoa kwa matabibu wa tiba mbadala
kuwasilisha taarifa za huduma zao.
Ahadi ya JPM ya ujenzi wa reli kuanza
Kigoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanza ziara mkoani Kigoma huku akiahidi
kuanza ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya viwango vya ‘standard gauge’,
itakayosaidia kuimarisha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka Dar es
Salaam kwenda nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC),
kupitia Bandari ya Kigoma.
Tamko
la Waziri Mkuu Majaliwa inaashiria kuanza kwa utekelezaji wa vipaumbele
25, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati, alivyovitoa Rais John Magufuli
(wakati huo akiwa mgombea urais wa CCM), Agosti 24, wakati wa uzinduzi
wa kampeni zake kwenye Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Mahakama yatupa pingamizi la ubunge dhidi ya Dk Mwakyembe
Waliokuwa wagombea ubunge, Jimbo la Vwawa, Fanuel Mkisi (wa pili kutoka kulia) na John Mwambigija (wa pili kushoto) wa jimbo la Rungwe, wote wa Chadema, wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya jana wakisubiri kusikiliza kesi zao walizofungua za kupinga matokeo yaliyowapa ushindi wagombea wa CCM katika majimbo hayo.
Mbeya. Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, imetupilia mbali shauri la kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe(CCM).
Kesi
ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo ilifunguliwa na
aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema, Abraham Mwanyamaki baada ya
kushindwa kulipa Sh3 milioni ambazo ni dhamana ya kesi kwa
anaowalalamikia.
Wanafunzi 70 wapoteza mwelekeo wa shule baada ya bomoabomoa Dar
PICHA:MWANANCHI
Dar es Salaam. Zaidi
ya wanafunzi 70 wa shule za msingi na sekondari huenda wakashindwa
kuendelea na masomo, baada ya familia zao kukumbwa na bomoabomoa kwenye
Bonde la Mto Msimbazi, na kukosa mahali pa kushi.
Zimeshapita
siku 12 tangu zaidi ya nyumba 300, zilizojengwa kwenye bonde hilo
zibomolewe na kulazimisha wakazi kuhamia sehemu nyingine na baadhi
kuishi juu ya vifusi.
Jumanne, 22 Desemba 2015
RAIS KAGAME AMPONGEZA MAGUFULI
Rais John Magufuli
akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya
mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu
Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli
kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa
Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari
kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji.
Rwanda, ambayo haijapakana na bahari, imekuwa ikiitegemea Bandari ya Dar
es Salaam kwa ajili ya kupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo yake.
Rais Kagame, ambaye miaka miwili ilkiyopita aliwahi kukosoa waziwazi
utendaji wa Bandari akieleza kuwa angepewa taasisi hiyo angeweza
kukusanya mapato ambayo yangeiendesha Tanzania, sasa anaonekana
kuridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano za kudhibiti mianya ya
kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi kwenye bandari
hiyo kongwe.
Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa
kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana,
Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame
alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa
Bandari.
Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa
Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi
zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo.
Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za
shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria
kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.
Mapema mwezi huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa
kushindwa kuwajibika ipasavyo kushughulikia matatizo ya Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
Pia, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe na kuagiza
uchunguzi dhidi yao uanze mara moja, alivunja Bodi ya Wakurugenzi TPA.
Kushirikiana na ADB
Katika hatua nyingine, Rais amemhakikishia mwakilishi mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (ADB), Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake
itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya kifedha katika utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na kumhakikishia ushirikiano,
Rais ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika
utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka
unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha
kutolewa.
Kwa upande wake, Dk Kandiero alisema benki hiyo iko tayari kuendelea
kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya
na kwamba kwa sasa imetenga Dola 2.3 bilioni kwa ajili ya kufadhili
miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Alisema ADB imelenga kujielekeza kutoa mikopo katika sekta ya nishati na
usafiri.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura
(kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha IkuluCopy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji.
Jumatatu, 21 Desemba 2015
Huyu ndiie Henricko (hk) ambae amepanga kufanya hiki katika mziki wake sikiliza na kudownload hapa
Msanii huyu ambae alivuma na kibao cha Wajanja ambae ni Henricko (hk) hivi sasa amepanga kufanya ngoma kali ya kufungia mwaka baada ya kutoa ngoma hii mpya alioifanya kwa C1 studio yaG.time na sasa kama bado
KINGWENDU ASEMA HIKI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA
Msanii wa vichekesho maarufu kama Kingwendu amewasihi vijana ambao wanatumia Madawa ya kulevya waachane nayo kwani ya naathali kubwa sana katika maisha ya binadamu,
Akizungumza na Thomas wikesi blogs Kingwendu amesema kuwa yeye anakuwa msitari wa mbele kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya .
Jumamosi, 12 Desemba 2015
Picha 3 za show ya Yamoto BAND Washington DC Marekani
Yamoto Band walisafiri kwenda Marekani kwa ajili ya shows kwenye miji mbalimbali na kukutana na Watanzania waishio Marekani ambao kwa kiasi kikubwa wamekua na kiu ya kuwaona kwenye stage Yamoto ambao ndio mara yao ya kwanza Marekani na hizi picha kwenye hii post ni za show yao ya Washington DC.
Mwakyembe Aomba Apewe Muda......Azungumzia Katiba Mpya
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ameapishwa leo na
rais John Magufuli kushika wadhifa huo amewaomba wadau na wananchi kwa
ujumla kumpa muda.
Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika
hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi
wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
KINANA AMVAA LOWASA ARUSHA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea
urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya
Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa).
TOURE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA BBC BARANI AFRIKA...................
Yaya Toure ndiye mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka 2015.
ROONEY ATAKIWA CHINA KWA GHARAMA KUBWA HAIJAWAHI KUTOKEA...........
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amepewa ya Pauni Milioni 75 kwenda kuungana na kocha Sven Goran Eriksson nchini China.
Jumanne, 8 Desemba 2015
HAYA SASA, HIZI NI ZILE TOP 5 STORIES ZA USAJILI WA DIRISHA DOGO ZINAZOTIKISA ULAYA
Dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya Ulaya litafunguliwa mwezi January ili kuvipa fursa baadhi ya vilabu kufanya usajili wa wachezaji kuimarisha vikosi vyao katika ligi mbalimbali ili kutafuta mafanikio au kufanya vizuri kwenye ligi hizo.
Kuna wachezaji na makocha mbalimbali wamekuwa wakitajwa au kuhusihwa na usajili huo unaosubiriwa na wadau wa soka kuona timu wanazozi-support zitafanya nini muda huo ukifika.
Hii hapa top 5 ya majina ya wachezaji na makocha yanayotajwa sana kwa sasa yakihusishwa kujiunga au kutemwa na baadhi ya
SCHWEINSTEIGER ATUPWA JELA YA FA
Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger 31, anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na chama cha soka England (FA) kutokana na kitendo chake cha kumpiga kiwiko usoni mlinzi wa Westham United, Winston Reid katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana Jumamosi iliyopita.
Schweinsteiger ana hadi Alhamis hii, saa sita mchana kukubali/kukataa kosa hilo baada ya FA kumuadhibu Jumatatu hii. Refarii Marc Clatternburg aliwaita wachezaji wote wawili na kuongea nao, huku asichukue hatua nyingine yeyote kutokana na kutoona tukio hilo.
PLUIJM HATAKI MCHEZO, AMPIGA CHINI MDOGOAKE MSUVA
Kama ulikua hujui sasa nakufanya ujue kuwa kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm hataki kabisa mchezo linapokuja suala la kazi, hii imemkuta kiungo wa timu hiyo James Msuva ambaye ni mdogo wa Simon Msuva baada ya kuachwa na kocha huyo wakati kikosi cha Yanga kikiingia kambini kujiandaa na mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Hizi ni rekodi za Messi ambazo hazijawahi vunjwa na mchezaji yoyote
Lionel Messi ni staa wa soka wa kimataifa wa Argentina ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania aliyojiunga nayo mwaka 2001 na mwaka 2003 akaanza kuichezea FC Barcelona C. Lionel Messi anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji soka wenye rekodi za kusisimua zaidi duniani. Hizi ni rekodi 5 za kusisimua za Lionel Messi stori kutoka sokkaa.com
5- Lionel Messi sio tu anatajwa kuwa mchezaji bora wa Dunia, ila wachambuzi wa masuala ya soka wanamuita ni moja kati ya wachezaji bora wa soka waliowahi kutokea katika historia ya soka. Messi ndio mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mara 4, kwani hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo.
Wasanii mbalimbali kutekeleza agizo la Rais MAGUFULI tarehe 9 December…..
Ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa awamo ya tano Dk.John Magufuli kutoa tamko la hakutakua na sherehe za kitaifa December 9 na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.
Sasa time hii headlines za usafi
zimewagusa wasanii na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda
ambapo tarehe 9 December wataungana kuhakikisha
Jumatatu, 7 Desemba 2015
Moto wa Rais Magufuli umeendelea bandarini, wengine wamesimamishwa leo..
Mpaka leo hii December 07 2015 tunahesabu kama mwezi mmoja hivi umepita tangu RaisMagufuli aapishwe na aanze kazi ya Urais wa awamu ya tano Tanzania.
Mfululizo wa stori zenye uzito wa kasi yake kwenye Urais zimekuwa zikitufikia kila siku, ya leo bado inabeba headlines za bandarini kwa mara nyingine… tangu siku ya kwanza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amefanya ziara ya ghafla bandarini mengi yameripotiwa ikiwemo ishu ya ubadhirifu
Alhamisi, 19 Novemba 2015
Hii ni Top 10 ya wachezaji wabunifu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza na adui wa Taifa Stars ndani …
November 18 nimekutana na list ya wachezaji wabunifu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza ila Top 10 hii iliyoandikwa na mtandao wa teamtalk.com
imetaja majina ya wachezaji 10
RAISI DK.MAGUFULI ATEUA JINA LA WAZIRI MKUU
Kikao cha Bunge kimeendelea Dodoma leo
November 19 2015, kikubwa kilichofanyika kwa siku ya leo ilikuwa ni
kutajwa kwa jina la Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania…
Jina lililoteuliwa na Rais Dk. Magufuli kushika nafasi hiyo ni la Mbunge wa Ruangwa, Majaliwa Kassim
Jumatano, 11 Novemba 2015
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 12, 2015 yameamka na hizi kwenye Udaku, Michezo na hardnews
SAMATTA AMUAHIDI KITU KIZURI RAIS MAGUFULI MGENI RASMI STARS V ALGERIA JUMAMOSI TAIFA
picha na Bin Zuber
WAKATI imetangazwa rasmi, Rais wa Jamhuri ya Dk John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Algeria, mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Mbwana Samatta amesema amepania makubwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake mchana wa leo mjini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, Saidy Mecky Sadick amesema kwamba Rais Magufuli ndiye mgeni rasmi katika mchezo huo.
Mecky Sadick amesema Rais huyo mpya wa awamu ya tano amekubali wito huo ili kujitokeza kuongoza kampeni ya kuwahasisha wachezaji wa Tanzania kuifunga Algeria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi.
Mbwana Samatta amempa ahadi nzuri Rais Dk John Pombe Magufuli kuelekea mchezo wa Taifa Stars na Algeria Jumamosi
Aidha, Samatta kwa upande wake amesema kwamba
Stori za Yanga kumsajili Hassan Kessy wa Simba, kuachwa Andry Coutinho majibu ndio haya
Ikiwa Ligi Kuu soka Tanzania bara imesimama kupisha mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Algeria na kupisha michuano ya Kombe la Challenge hadi December 12, homa ya dirisha dogo la usajili imeanza kwa vilabu kadhaa kuanza kuhusishwa kunyemelea saini za wachezaji.
Baada ya kocha mkuu wa Simba kutoelewana na msaidizi wake, haya ndio maamuzi ya Matola …
Klabu ya soka ya Simba inayonolewa na kocha muingereza Dylan Kerr huku msaidizi wake akiwa Selemani Matola
imezidi kuingia katika headlines baada ya zile tetesi za muda mrefu
kuthibitika rasmi usiku wa November 11, awali kulikuwa na stori za
mahusiano yasio mazuri kati ya kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr na msaidizi wake Selemani Matola
TOTO AFRICANS YAITISHA MKUTANO WA DHARURA
Jumanne, 10 Novemba 2015
CHALLENGE CUP: KILIMANJARO STARS YAPANGWA NA WENYEJI
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)